Wazazi Wametakiwa kuwafikisha Watoto wenye matatizo ya Minguu rungu Hospitali.

P 1Wazazi wa Watoto wenye Miguu Rungu (Clubfoot) Wametakiwa kuwafikisha Watoto wenye matatizo hayo Hospitali kwa ajili ya matibabu ili kuwaepusha na ulemavu wa kudumu.

Hayo ameyasema Mtabibu wa Miguu Rungu ambae pia ni Mtaalamu wa Viungo Bandia ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja Dr. Adil Mussa Haroun amesema kuna baadhi wa wazazi huwafungia ndani watoto wenye matatizo ya miguu rungu na kutowapeleka Hospitali na kudhani kuwa ni ulemavu jambo ambalo sio la kweli kwani tatizo la miguu rungu hutibika na kuondoka kabisa.

 Pia amesema kwa asilimia kubwa tayari watu washaanza kuwa na uwelewa kwani jitihada zao za kutoa mafunzo katika maeneo mbali mbali ya mjini na vijijini kuhusiana na kuwepo kwa Watoto wenye miguu rungu(Club foot) watu hupata muamko na kuwapeleka Watoto wao Hospitali ya Mnazi mmoja kwaajilio ya matibabu.

Hata hivyo amewatoa hofu wazazi kua matibabu yote pamoja na vifaa vya kuwa weka sawa Watoto vinapatikana hospitalini hapo bila ya gharama yoyote .

Kila ifikapo 3 June ya kila mwaka huwadhimisha siku ya miguu rungu(Club foot) duniani lengo ni kutoa elimu na huduma nzuri katika jamiii, ambapo kwa mwaka huu imekuja na kauli mbiu inayosema ‘‘Miguu Rungu si ulemavu kwa hakika inatibika’’.

Read 1086 times Last modified on Thursday, 24 February 2022 13:40
Rate this item
(0 votes)

Partners

Social media

f  I

Mnazi Mmoja Hospital map Location

Contact us

Mnazi Mmoja Hospital

Stone Town-Vuga Street

P.O.BOX 672

Tel: +255773833768 / +255627600600

Fax: +255 24 2231613

Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Web: www.mmh.go.tz