Kuwepo kwa vifaa vya kutosha na Madaktari Bingwa katika kitengo katika cha Macho kutaboresha huduma za kimatibabu kwa urahisi kwa Wagonjwa wetu.
Hayo yameelezwa na Daktari Mkuu wa Kitengo cha Macho ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Dk Slim Mohammed Mgeni katika siku ya kufunga kambi ya matibabu ya macho kwa Watoto.
Kambi hiyo imefadhiliwa kwa udhamini wa lions club -mzizima Dar-es salam kwa lengo la kutoa huduma za kimatibabu na kuisaidia jamii kupata matibabu ya macho kwa Watoto bila malipo.
Aidha Dk, Slim amesema wagonjwa waliopatiwa matibabu walikua 360 kwa maradhi tofauti yakiwemo presha ya macho,kensa ya macho,makengeza,macho yanayohitaji miwani na maradhi mengine ya macho ikiwemo kufanyiwa upasuaji kwa waliohitaji huduma hiyo.
Nae Muakilishi wa Jumuiya iyo ya Lions club Mohamed Rasulullah kwa niaba ya Jumuiya hiyo amesema wameona ni vyema kutoa huduma ya macho bila malipo kwani Watoto wengi hupata matatizo na baadae wazazi kushindwa kuwahudumia Watoto wao ndio maaana wameamua kutoa huduma hiyo kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka hospitali ya Muhimbili Pamoja na madaktari bingwa wa hospitali ya mnazi mmoja.
Muakilishi wa Jumuiya ya Lions club Mohamed Rasulullah akitoa neno la shukurani kwa Uongozi wa HOSPITALI kwa namna walivyopata mashirikiano katika kipindi chote cha KAMBI ya matibabu hayo.
Dakitari mkuu wa Kitengo cha Macho Dk. Slim amesema wamefanya matibabu hayo kwa lengo la kuwapunguzia mzingo mkubwa wa gharama kubwa za matibabu ya macho.