Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Hussein Ali Mwinyi amempongeza mwekezaji mzalendo Mohamed Abdallah Mohamed ambae pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Zanzibar Cable Television kwa kujitolea kujenga jengo la kuhifadhia maiti MOYUARY katika Hospitali ya Mnazi mmoja.
Dr. Mwinyi amesema juhudi za muekezaji huyo zimechochea ari na hamasa ya wafanyabiashara wenzake na wananchi wengine kujitolea kutoa misaada ya kijamii.
Amesema ujenzi huo wa chumba cha kuhifadhia maiti chenye majokofu Matano na uwezo wa kuhifadhi maiti 20 kwa wakati mmoja unathaminiwa sana ambapo kutaweza kuhifadhiwa maiti kunapotokezea majanga mbali mbali ikiwemo vifo vyenye utata na ajali.
Daktari bingwa wa vifo vinavyotokana na Jinai Dr. Wardat Attai Masoud amesema Hospitali imekuwa na jukumu kubwa la kufanya upasuji wa vifo vyenye utata, ajali na vile vinavyotokana na jinai kwa kiasi kukibwa kutokana na engezeko la kesi hizo na kwa wale ambao bado hawajajulikana jamaa zao huhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mnazi mmoja ambacho kilikua na changamoto kadhaa hivyo kuwepo kwa jingo hilo lenye maeneo ya nafasi litasaidia kwa kiasi kikubwa kwa hospitali.
Mh.Waziri wa Afya Usitawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Bwana Nassor Ahmed Mazorui amesema sasa hospitali imeshakuwa na nafasi yakutosha ya kuhifadhi Maiti, maiti zinaweza kuhifadhiwa vizuri.