Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dr.Hussein Mwinyi ameipongeza taasisi ya LADY FATMA FOUNDATION kwa msaada wake wa huduma ya maji katika Hospitali ya Mnazi mmoja .
Dr. mwinyi alisema kuwa ni Habari njema kuona kuwa kupitia mradi huo sasa hospitali inauwezo wa kuzalisha lita 240,000 kwa siku moja ikiwa mahitaji ni lita 400,000 ambapo tayari umeshaipunguzia mzigo mkubwa mamlaka ya maji Zanzibar ZAWA hasa pale miundombinu ya maji inapoharibika.
Rais Dr. Mwinyi alitoa pongezi kwa taasisi hiyo kwa kuratibu na kutafuta wafadhili wa mradi huo na kuchimba visima, pia aliipongeza kampuni ya DEG ya Ujerumani kwa kuleta Mitambo ya kuchuja chumvi na Mitambo ya kuzalisha umeme wa jua ambao utatumika katika Mtambo huo wa kusafisha maji chumvi na kuwa maji salama.
Waziri wa Afya, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amesema mtambo huo umekuja muda muafaka kutokana na kuwepo upungufu wa maji kutoka ZAWA na kupelekea hospitali kuwa na upungufu wa maji hivyo kuchimbwa kwa Visima hivyo Pamoja na kuwepo kwa mtambo wa kuchujia maji ya chumvi na kuwa maji salama utasaidia sana upatikaji wa maji ndani ya Hospitali.