SERIKALI YA MAPIDUZI ZANZIBAR YA AWAMU YA NANE INADHAMIRA YA DHATI KABISA YA KUJENGA KITUO KIPYA CHA MARADHI YA SARATANI KWA VIFAA BORA VYA UHAKIKANA VYA KISASA.
AMEYASEMA HAYO WAZIRI WA AFYA USTAWI WA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO MHE.NASSOR MAZRUI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA SARATANI DUNIANI DUNIANI (WORLD CANCER DAY) YALIYOFANYIKA KATIKA KITENGO CHA MARADHI YA SARATANI NDANI YA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA.
AMESEMA LENGO LA MAADHIMISHO HAYO NI KUKAA KWA PAMOJA NA WATAALAMU WA MARADHI HAYO NA KUJUA NAMNA YA KUJIKINGA NA MARADHI YA SARATANI KWANI KINGA NI BORA KULIKO TIBA.
HATA HIVYO AMEWAOMBA WANANCHI WANAPOHISI HALI YA UTOFAUTI KATIKA MWILI AU UVIMBE WOWOTE WAFIKE KITUO CHA AFYA KWAAJILI YA UCHUNGUZI.
NAE MKURUGENZI MTENDAJI WA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA AMBAE PIA NI DAKTARI BINGWA WA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA SARATANI MSAFIRI L. MARIJANI, AMEELEZA UGONJWA WA SARATANI NI UGONJWA UNAOCHUKUA NAMBA MBILI DUNIANI UNAOPELEKEA KIFO KWA MUATHIRIKA HIVYO HOSPITALI INAJITAHIDI KWA KIASI KIKUBWA KUTIBU UGONJWA HUO KWA MUDA MUAFAKA INGAWA GHARAMA ZA VIPIMO NA MATIBABU KWA WAGONJWA WA SARATANI NI KUBWA SANA.
AMEISHAURI JAMII IWE NA UTARATIBU WA KUCHANJA CHANJO HUSUSANI CHANJO DHIDI YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WASICHANA WENYE UMRI KUANZIA MIAKA 13 ILI KUUWA BAKTERIA WANAOATHIRI SHINGO YA KIZAZI.
MUAKILISHI WA BALOZI WA NCHINI UTURUKI KUTOKA TANZANIA BARIS OZYURT AMBAE NI MKURUGENZI WA TUKRISH MAARIF SCHOOL,AMEWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUPATIWA HUDUMA YA KIMATIBABU PIA AMETAJA VIDOKEZO VINAVYOPEKEA KUPATA UGONJWA WA SARATANI ,UNENE ULIOKITHIRI,UKOSEFU WA MAZOEZI,UTUMIAJI WA TUMBAKU,POMBE NA JAMBO KUBWA LA MSONGO WA MAWAZO(STRESS)
MAADHIMISHO YA SIKU YA SARATANI DUNIANI HUAZIMISHWA KILA KILA IFIKAPO FEBRUARI 04 YA KILA MWAKA AMBAPO KAULI MBIU YA MWAKA HUU…IMARISHA HUDUMA ZA SARATANI ZIWAFIKIE WOTE.